MUASISI wa filamu msanii Mahiri katika filamu za mapigano Tanzania
Jimmy Mponda ‘Jimmy Master’ anasema kuwa moja ya sifa au ubora wa kazi
zake kudumu kwa muda mrefu ni kutokana na umakini, ubora na matumizi ya
gharama katika uaandaaji wa filamu zake hatumii muda mfupi kutayarisha
filamu.
.
.
“Filamu
zangu zinatumia gharama kubwa katika kuandaa lakini kitu kingine ni
muda wa kutosha kwani toka niingie katika uandaaji wa filamu sijawahi
chini ya miezi sita na kuendelea, sinema za mapigano ni ngumu lazima
ujue martial arts somo ambalo mimi ni mwalimu,”anasema Jimmy Master.
Jimmy ndiyo muasisi wa filamu za Kibiashara sinema nchini yake ya
kwanza Shamba kubwa alirekodi mwaka 1995 akishirikiana na Kaini Jijini
Tanga, filamu nyingine ni Kifo Haramu, Misukosuko, Double J, na filamu
nyingi na sinema za Jimmy ni tofauti sana na nyingine zinatoka kwa
matoleo zaidi ya nne kama ilivyo Double J 1,2,3,4 na 5 Final.Maelezo ya stori hii yanatoka katika gazeti moja , nilipokuwa nikihojiwa na
chombo hicho sikuchache zilizopita.