Mzimuni

Monday, October 14, 2013

NATUMIA GHARAMA KUBWA KUANDAA FILAMU ZANGU-JIMMY MASTER


Jimmy Mponda
Jimmy Master mtayarishaji wa filamu Swahilihood.
MUASISI wa filamu msanii Mahiri katika filamu za mapigano Tanzania Jimmy Mponda ‘Jimmy Master’ anasema kuwa moja ya sifa au ubora wa kazi zake kudumu kwa muda mrefu ni kutokana na umakini, ubora na matumizi ya gharama katika uaandaaji wa filamu zake hatumii muda mfupi kutayarisha filamu.

.
Jimmy mponda
Jimmy Master akiwa katika pozi la mazoezi ya kimapigano
Jimmy Mponda 560
Jimmy Mponda 566 

“Filamu zangu zinatumia gharama kubwa katika kuandaa lakini kitu kingine ni muda wa kutosha kwani toka niingie katika uandaaji wa filamu sijawahi chini ya miezi sita na kuendelea, sinema za mapigano ni ngumu lazima ujue martial arts somo ambalo mimi ni mwalimu,”anasema Jimmy Master.
Jimmy ndiyo muasisi wa filamu za Kibiashara sinema nchini yake ya kwanza Shamba kubwa alirekodi mwaka 1995 akishirikiana na Kaini Jijini Tanga, filamu nyingine ni Kifo Haramu, Misukosuko, Double J, na filamu nyingi na sinema za Jimmy ni tofauti sana na nyingine zinatoka kwa matoleo zaidi ya nne kama ilivyo Double J 1,2,3,4 na 5 Final.Maelezo ya stori hii yanatoka katika gazeti moja , nilipokuwa nikihojiwa na
chombo hicho sikuchache zilizopita.

No comments:

Post a Comment